Kilengilu

Kilengilu ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Walengilu kwenye kisiwa cha Kalimantan. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kilengilu imehesabiwa kuwa wazee watatu tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kilengilu iko katika kundi la Kiborneo-Kaskazini.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search