Wataveta

Wataveta ni kabila la watu (20,000 hivi) wa jamii ya Wabantu wanaoishi kusini mwa Kenya, katika kaunti ya Taita-Taveta, mpakani mwa Tanzania.

Lugha yao ni Kitaveta, mojawapo kati ya lugha za Kibantu, lakini wengi wanaongea pia Kiswahili. Lugha ya Kitaveta inafanana kwa zaidi ya asilimia 95 (95%) na lugha ya Kipare.

Baadhi ya majina na koo za Wataveta zinafanana na majina na koo za Wapare wa Tanzania, mfano majina kama Senzia, Mcharo, Semboja n.k. yapo kwa Wataveta na pia kwa Wapare. Koo kama Msuya, Mziray, Mrutu n.k. zipo kwa Wapare na Wataveta pia.

Wengi wao ni Wakristo na Waislamu.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search