Zangalewa

Zangalewa (Zamina mina, kwa jina lingine) ni wimbo uliorekodiwa mwaka wa 1986 na kikundi cha densi cha Zangalewa (Bendi la Muziki). Wimbo huu unajulikana nchi karibu zote za Afrika, na kutumiwa na skauti, polisi na wanajeshi wa nchi hizo haswa katika mazoezi yao. Umeimbwa katika lugha kadhaa zinazopatikana nchi za Afrika Magharibi.

Katika lugha ya Kiduala, maana ya "Zangalewa?" ni "Nani alikuita?", ama, "Nani alikuambia uingie kwenye jeshi?"


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search