Al Jazeera

Al Jazeera English ni stesheni ya runinga ya kutangaza habari na taarifa za mambo leo masaa ishirini na nne kwa lugha ya Kiingereza iliyo na makao yake makuu ni mjini Doha, Qatar.

Nembo ya Al Jazeera

Stesheni hii huonyesha habari za makala na uchambuzi, mijadala, taarifa za mambo leo, biashara, teknolojia, na michezo. Wao hudai kuwa stesheni ya kwanza ya kimataifa inayotangaza kwa mtandao wa kisasa (high-definition).[1] Kauli yake mbiu ni Setting the News Agenda.

Hii ni stesheni ya kwanza inayotangaza kwa lugha ya Kiingereza iliyo na makao yake makuu kwenye nchi iliyo Mashariki ya Kati.[2]

Al Jazeera ina vituo vinne vikuu kote duniani, mjini London, Washington, DC, Kuala Lumpur na Doha. Ina milikiwa na serikali ya Qatar.[3] Hii ni moja kati ya stesheni chache iliyo na ofisi zake mjini Gaza na Harare.

  1. Fact and Figures, iwantaje.com
  2. Al-Jazeera says its English-language news channel will launch November 15, The Post-Star published 1 Novemba 2006
  3. Owned by Qatari Government

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search