| |||||
Kaulimbiu ya taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Azərbaycan Respublikasının Dövlət Himni | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Baku | ||||
Mji mkubwa nchini | Baku | ||||
Lugha rasmi | Kiazeri | ||||
Serikali | Jamhuri Ilham Aliyev (İlham Əliyev) Ali Asadov (Əli Əsədov) | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilikamilishwa |
30 Agosti 1991 25 Desemba 1991 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
86,600 km² (ya 112) 1.6 | ||||
Idadi ya watu - 2019 kadirio - 1999 sensa - Msongamano wa watu |
10,097,171[1] (ya 91) 7,953,438 115/km² (ya 99) | ||||
Fedha | Manat (AZN )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+4) (UTC+5) | ||||
Intaneti TLD | .az | ||||
Kodi ya simu | +994
- |
Azerbaijan pia Azebajani rasmi kama Jamhuri ya Azerbaijan, ni nchi katika Kaukazi, inayopakana na Bahari ya Caspian mashariki, Urusi kaskazini, Georgia kaskazini-magharibi, Armenia magharibi, na Iran kusini. Ina idadi ya watu takriban milioni 10, ikiwa ya 90 duniani. Jiji lake kubwa zaidi ni Baku, ambalo pia ni mji mkuu. Azerbaijan imegawanyika katika majimbo 66 na miji huru 11.
Azerbaijan ni pia jina la mikoa miwili magharibi mwa Uajemi (Azerbaijan ya Mashariki na Azerbaijan ya Magharibi); nchini Uajemi takriban 16% za wakazi ni Waazeri; kwa jumla walioko Uajemi ni wengi kushinda walioko Azerbaijan yenyewe.
Eneo la Nakhichevan ni sehemu ya Azerbaijan inayopakana na Uturuki na Uajemi lakini imetenganika na sehemu kubwa ya nchi kwa sababu katikati kuna eneo la Armenia.
Eneo la Nagorno-Karabakh linalokaliwa na Waarmenia ndani ya Azerbaijan lilijitangaza nchi huru mwaka 1991 lakini haijatambuliwa na umma wa kimataifa.
Azerbaijan ni nchi mwanachama wa baraza la Ulaya tangu mwaka 2001. Hivyo kisiasa inahesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya, lakini kijiografia mara nyingi yahesabiwa kuwa sehemu ya Asia ya Magharibi.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search