Bahari ya Eire

Ramani ya Bahari ya Eire (Irish Sea).

Bahari ya Eire (kwa Kiingereza: Irish Sea) ni sehemu ya bahari inayotenganisha visiwa vya Eire (Ireland) na Britania.

Ndani yake kuna visiwa viwili vikubwa kiasi ambayo ni Anglesey (Welisi) na Isle of Man, pamoja na visiwa vidogo.

Inapakana na nchi za Welisi, Uingereza na Uskoti (zote sehemu za Ufalme wa Muungano) upande wa mashariki, halafu Eire na Eire ya Kaskazini (pia sehemu ya Ufalme wa Muungano) upande wa magharibi.

Kila mwaka kuna abiria milioni 12 wanaovuka bahari hii na bidhaa tani milioni 17 zinasafirishwa kati ya Britania na Eire.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search