Bamba la Karibi

Bamba la Karibi
Volkeno za Karibi

Bamba la Karibi ni bamba la gandunia lililopo chini ya Amerika ya Kati na Bahari ya Karibi. Limepakana na mabamba ya Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini na Nazi (Cocos Plate). Eneo lake ni takriban milioni 3.2 km².

Mipaka yake na mabamba mengine ni mahali pa matetemeko ya ardhi na milipuko ya volkeno. Baharini mpaka huu unaonekana kwa pinde la visiwa vya Karibi.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search