Bandari

Bandari kuu za dunia
Kwenye bandari ya Singapur
Bandari ya Hamburg huwa na winchi za upakizaji za kisasa kabisa

Bandari ni mahali pa kupokea meli na kuhamisha mizigo yao pamoja na abiria. Bandari inatakiwa kuipa meli kinga dhidi ya mawimbi makubwa na vifaa ya kupakiza au kutoa mizigo. Kuna bandari asilia na bandari zilizotengenezwa kwa kusudi hii. Kwa jumla bandari ni sehemu muhimu za miundombinu wa nchi.

Bandari hutengenezwa kando ya bahari, maziwa au mito.

Kati ya sifa muhimu kwa ajili ya bandari ni

  • kina cha maji cha kutosha kulingana na ukubwa wa meli zinazoitumia.
  • mitambo kama winchi za upakizi
  • nafasi za ghala
  • njia za usafiri kama reli na barabara za kusafirisha mizigo

Bandari hutofautiana kulingana na kusudi lao na aina za mizigo inayoshughulikiwa humo.

Bandari ndogo zinahudumia wavuvi au jahazi za burudani.

Kuna bandari zinazopokea mizigo ya kila aina kama bandari ya Dar es Salaam au Mombasa.

Mara nyingi kuna bandari zinazoshughulikia mizigo maalumu kama mafuta, kontena, kivuko na kadhalika.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search