Basseterre

Basseterre

Mji wa Basseterre (Saint Kitts na Nevis)
Habari za kimsingi
Utawala Shirika raia za Saint George na Saint Peter
Anwani ya kijiografia Latitudo: 17°18′N
Longitudo: 62°44′W
Kimo 15 m juu ya UB
Eneo 6.1 km²
Wakazi - mji: 15,500 (2005)
Msongamano wa watu watu 2,541 kwa km²
Simu +1869 (nchi yote)
Mahali

Basseterre ni mji mkuu wa shirikisho la Saint Kitts na Nevis ambalo ni nchi ya visiwani ya Antili Ndogo kwenye Bahari Karibi. Idadi ya wakazi ni takriban 15,500 (2005).

Mjini kuna kitovu cha kiuchumu wa visiwa, uwanja wa ndege na viwanda vya sukari.

Mwimbaji Joan Armatrading alizaliwa Basseterre kabla ya kuhamia Uingereza na wazai wake akiwa mtoto.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search