Berlin






Berlin

Bendera

Nembo
Berlin is located in Ujerumani
Berlin
Berlin

Mahali pa mji wa Berlin katika Ujerumani

Majiranukta: 52°30′2″N 13°23′56″E / 52.50056°N 13.39889°E / 52.50056; 13.39889
Nchi Ujerumani
Jimbo Berlin
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 3,878,100 (2,023)[1]
Tovuti:  www.berlin.de
Mji wa Berlin

Berlin ni mji mkuu, pia mji mkubwa na jimbo la kujitawala la Ujerumani ikiwa na wakazi zaidi ya 3.8 milioni. Berlin iko mashariki mwa Ujerumani, palipo mto unaoitwa Spree.

Berlin ilianza kukua kama mji mkuu wa Prussia, ikawa mji mkuu wa Ujerumani tangu kuundwa kwa Dola la Ujerumani mwaka 1871. Kati ya miaka 1949 na 1991 ilikuwa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani.

Kati ya miaka 1961 na 1989 mji ulitengwa na ukuta kati ya sehemu za mashariki na magharibi. Baada ya kuungana tena kwa Wajerumani mnamo 1990, Berlin ikawa tena mji mkuu wa Ujerumani yote.

  1. Amt für Statistik Berlin-Brandenburg Einwohnerbestand in Berlin – Grunddaten 31. Dezember 2023, halbjährlich

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search