Eneo la kudhaminiwa

Maeneo ya kudhaminiwa
1 Syria (Ufaransa) - 2 Lebanon (Ufaransa) – 3 Palestina (Uingereza) – 4 Ng’ambo ya Yordani (Uingereza) - 5 Irak ((Uingereza) - 6 Togo (Uingereza) - 7 Togo (Ufaransa) – 8 Kamerun (Uingereza) - 9 Kamerun (Ufaransa) - 10 Ruanda-Urundi (Ubelgiji) - 11 Tanganyika (Uingereza) - 12 Afrika ya Kusini-Magharibi (Afrika Kusini)

Eneo la kudhaminiwa lilikuwa eneo lililokabidhiwa na umma wa kimataifa mikononi mwa nchi iliyotakiwa kulisimamia. Katika karne ya 20 maeneo ya kudhaminiwa yalikuwa aina ya pekee ya ukoloni. Utawala wa mkoloni ulitekelezwa rasmi kwa niaba ya nchi huru zote za Dunia. Hali hii ya pekee ilikuwa na umuhimu hasa wakati wa uhuru wa nchi hizo.

Maeneo hayo yalianzishwa mwaka 1919 katika Mkataba wa Versailles uliounda Shirikisho la Mataifa lililokuwa mtangulizi wa Umoja wa Mataifa wa leo.

Nchi tawala za maeneo ya kuadhiminiwa zilipokea maeneo yale chini ya masharti ya katiba ya Shirikisho la Mataifa zikatakiwa kutoa taarifa za kila mwaka na kuyaandaa kwa uhuru wa kisiasa.

Hali halisi maeneo ya kudhaminiwa yalitendewa kama makoloni ya kawaida kwa miaka mingi.

Baada ya mwaka 1945 Shirikisho la Mataifa lilikwisha na usimamizi mkuu ulipitia mikononi mwa Umoja wa Mataifa. Wakati ule jina la maeneo ya kudhaminiwa kwa lugha ya Kiingereza likabadilishwa, kutoka "mandate" au "mandated territory" kuwa "trust territory", lakini maana ya maneno haya ni yaleyale.

Maeneo yote yamepata uhuru. Mfano wa pekee ni Israel na Palestina ambako hadi leo hakuna utaratibu wa kudumu katika eneo la kudhaminiwa la zamani.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search