Frigia

Ramani inayoonyesha Frigia katika rasi ya Anatolia.

Frigia (kwa Kiing. Phrygia) ni jina la ufalme wa zamani, halafu mkoa wa milki mbalimbali zilizotawala Anatolia ambayo leo hii inaunda sehemu kubwa ya nchi ya Uturuki.

Kati ya wafalme mashuhuri wa Frigia alikuwepo Midas anayekumbukwa kama tajiri kwa sababu inasimuliwa kwamba kila kitu alichokigusa kilibadilika kuwa dhahabu.

Mji mkuu wa Frigia ilikuwa Gordion; mabaki yake yamegunduliwa na wanaakiolojia karibu na mji wa Eskishehir. Aleksander Mashuhuri alipita huko akakuta "fundo la Gordion" lililofanywa na kamba la kushika gari kwenye hekalu la mji; kulikuwa na utabiri uliosema "atakayefungua fundo hilo atatawala Asia". Aleksander alipopita akaangalia fundo akatoa upanga wake na kukata fundo.

Wakazi walioitwa Wafrigia walitokea Ulaya na kuzungumza lugha iliyofanana kidogo na Kigiriki.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search