Guadeloupe

Guadeloupe,Ufaransa








Guadeloupe

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Ufaransa Ufaransa
Mji mkuu Basse-Terre
Eneo
 - Jumla 1,628 km²
Idadi ya wakazi (2016)
 - Wakazi kwa ujumla 394,110
Tovuti:  http://www.cr-guadeloupe.fr/
Maeneo mweupe ni sehemu za Guadeloupe

Guadeloupe ni eneo la ng'ambo na mkoa (departement) wa Ufaransa katika Bahari ya Karibi lenye visiwa tisa vidogo. Hivyo ni sehemu ya Umoja wa Ulaya.

Makao makuu ni Basse-Terre, ingawa mji mkubwa ni Pointe-à-Pitre.

Wakazi asilia walikuwa Waindio. Utamaduni wao uliharibiwa kabisa kwa kuja kwa ukoloni kutoka Ulaya (1493).

Ilikuwa koloni la Ufaransa halafu la Uingereza halafu la Uswidi halafu la Ufaransa tena.

Eneo lake ni km² 1,628.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search