Harambee

Harambee ni neno ambalo lilitungwa na hayati Mzee Jomo Kenyatta (rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya) ili kuwapa motisha wafanyakazi na hasa wale wanaofanya kazi nzitonzito.

Harambee hutoka kwa neno la Kihindi, Har Ambee, ambalo ni sifa kwa miungu wa kihindi wawape nguvu na uwezo wa kufanya kazi.

Neno hili lilisikika sana wakati wahindi walitumiwa kama vibarua wa kutengeneza reli kati ya Nairobi na Mombasa.

Kisha likatoholewa na mwishowe likaja kujulikana kumaanisha "tuvute pamoja"


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search