Jumuiya ya Madola

Jumuiya ya Madola (Commonwealth of Nations)


Bendera ya Jumuiya ya Madola

Lugha rasmi Kiingereza
Katibu Mkuu Don McKinnon (tangu 1999)
Chanzo chake mw. 1926 kama jumuiya ya "Kibritania", tangu 1949 kama Jumuiya ya Madola ya kisasa
Madola wanachama 53
Makao Makuu Westminster, London
Mtandao thecommonwealth.org

Jumuiya ya Madola (jina la Kiingereza ni Commonwealth of Nations) inaunganisha nchi mbalimbali hasa Uingereza na nchi zilizokuwa koloni zake.

Umoja huu umeanzishwa mw. 1926 kama "Jumuiya ya Kibritania" (British Commonwealth) na kupewa jina lake la sasa tangu 1949. Inafuatana na Dola la Kibritania au Dola la Kiingereza ambayo ilikuwa dola kubwa kabisa katika historia ya dunia lakini maeneo yake yalianza kuachana baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia kutokana na kudhoofishwa kwa Uingereza vitani na miendo ya kupigania uhuru katika nchi mbalimbali hasa Uhindi.

Leo zipatao asilimia 30 ya watu wote duniani (watu 1,800,000) huishi katika nchi wanachama za Jumuiya ya Madola. Nchi za jumuiya hii wenye wakazi wengi ni hasa Uhindi, Pakistan, Bangladesh na Nigeria. Kuna pia nchi ndogo sana kama Tuvalu yenye wakazi 11,000 pekee.

Nchi kadhaa zilisimamishwa uanachama au kuondoka kwa hiari zao. Mfano Tanganyika na Zanzibar ziliungana kwa hiyo hazipo tena lakini mpya ya Tanzania imekuwa nchi mwanachama. Vilevile Newfoundland iliondoka katika jumuiya baada ya kujiunga na Kanada kama jimbo.

Pakistan ilisimamishwa uanachama mara kadhaa kwa sababu serikali yake ilipinduliwa na wanajeshi walioanzisha serikali ya kijeshi. Imerudishwa tena.

Zimbabwe ilisimamishwa uanachama baada ya uchaguzi bandia 2002 ikaamua kujiondoa kabisa mwaka 2003.

Jamhuri ya Ueire iliamua mwaka 1949 kuacha viungo vyote na Uingereza ikajitangaza kuwa jamhuri isiyokubali athira ya nje kama hali ya malkia wa Uingereza kuwa mkuuw a dola hivyo ikaondoka katika jumuiya.

Afrika Kusini ilijiondoa 1961 kwa sababu ya upinzani wa jumuiya dhidi ya sheria za apartheid. Baada mwisho wa ubaguzi wa rangi nchi ilirudi katika jumuiya.

Fiji imesimamishwa mara kadhaa baada ya uasi wa kijeshi uliopindua serikali.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search