Kabati

Picha ya kabati ya kioo.

Kabati (kutoka Kiingereza "cup-board") ni samani ambayo watu huitumia kuhifadhia vitu, kwa mfano: vyombo, nguo, mabeseni na midoli.

Kwa kawaida kabati linawekwa ofisini, sebuleni, jikoni, bafuni n.k.

Kwa kawaida ina rafu moja au zaidi ya kuweka vitu, pia inaweza kuwa na mlango wa mbao, chuma au kioo.

Kabati inaweza kutumika pia kama kitu cha mapambo katika nyumba.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search