Kalenda ya jua

Gari la Jua lilitengenezwa kwa hekalu ya Kigermanik katika Denmark miaka 3500 iliyopita. Wazee wale waliwaza kuwa jua linavutwa kwa gari angani. Kutazama jua kulikuwa mwanzo wa kalenda.

Kalenda ya jua ni kalenda inayofuata mwendo wa jua jinsi inavyoonekana angani. Hali halisi tunaona matokeo ya mwendo wa dunia kuzunguka jua.

Katika kalenda za jua mwaka unalingana na muda wa mzunguko mmoja wa dunia kwenye mzingo wake kuzunguka jua letu. Muda kamili wa mzunguko huu ni siku 365.2425.

Kwa kawaida kalenda za jua hutumia mwaka mwenye siku 365 na kuongeza siku moja kila baada ya miaka minne au kwa utaratibu mwingine.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search