Kanuni ya Imani ya Mitume

Mchoro wa karne ya 13 ukionyesha Thenashara wakiandika Kanuni ya Imani, ilivyosadikika wakati huo.


Kanuni ya Imani ya Mitume (kwa Kilatini: Symbolum Apostolorum au Symbolum Apostolicum) ni ungamo la imani ya Ukristo lililoanza kutumika mjini Roma katika karne ya 2 kwa ajili ya ubatizo, halafu likaenea hasa katika Kanisa la Magharibi.[1]

Kanuni hiyo inaendelea kutumiwa na Kanisa Katoliki na madhehebu mengi ya Uprotestanti katika liturujia na katekesi.

Kwa kuwa ilitokea Ulaya Magharibi, ambapo elekeo la kinadharia si kubwa kama huko Ugiriki, tena mapema kuliko mabishano mengi ya teolojia kuhusu umungu wa Yesu Kristo na wa Roho Mtakatifu, haina ufafanuzi wa kina.

Maandishi ya zamani zaidi tuliyonayo yanayoitaja "Kanuni ya Imani ya Mitume" ni barua ya mwaka 390 hivi kutoka sinodi ya Milano kwa Papa Siricius.[2][3][4]

  1. Neno la Kilatini symbolum, ishara, zawadi, linatokana na Kigiriki σύμβολον, kutoka kitenzi συμβάλλειν, kuweka pamoja, kulinganisha" (The American Heritage Dictionary of the English Language).
  2. Jack Rogers, Presbyterian Creeds (Westminster John Knox Press 1985 ISBN 978-0-664-25496-4), pp. 62–63
  3. "James Orr: The Apostles' Creed, in International Standard Bible Encyclopedia". Reformed.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-22. Iliwekwa mnamo 2011-05-19. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. "Apostles Creed". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-12. Iliwekwa mnamo 2014-09-21.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search