Kioo

Stempu ya mwaka 1921 ikionyesha utengenezaji wa kioo.

Kioo ni dutu imara na ngumu inayopatikana kwa umbo lolote. Kwa kawaida ni kiangavu na wazi maana yake kinaruhusu kuona yale yaliyopo nyuma yake. Inatengenezwa pia kwa rangi mbalimbali kwa mfano kwa ajili ya madirisha ya makanisa. Kioo ni dutu hobela, hakina fuwele ndani yake.

Matumizi ya kila siku ni katika chupa na madirisha ya kioo.

Kioo hutokea kiasili kama silika, inapashwa joto kali zaidi ya sentigredi 2,000. Watu walikuta kioo cha aina hiyo baada ya milipuko ya volkeno au moto asilia mkali. Walijifunza kuitengeneza kwa kuongeza viungo kadhaa vinavyopunguza kiwango cha kuyeyuka.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search