Kios

Nea Moni.

Kios (kwa Kigiriki: Χίος, Khíos) ni kisiwa cha Ugiriki katika Bahari ya Aegean.

Kina wakazi 51,930 (2011) wanaotegemea zaidi uvuvi na utalii.

Monasteri ya Nea Moni (karne ya 11) imeorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.

Kinatajwa na Biblia ya Kikristo kwa kuwa mwaka 58 Mtume Paulo, katika safari yake ya tatu ya kimisionari, aliabiri kutoka Lesbo hadi Samos akipitia huko (Matendo ya Mitume 20:15).


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search