Kipapiamentu

Kipapiamentu (kwa Kiingerezaː Papiamento) ni lugha ya visiwa kadhaa vya Karibi (hasa Aruba, Bonaire na Curaçao) inayotumiwa na watu 341,300[1].

Ni krioli iliyotokana na Kireno (na Kihispania) na inafanana na krioli ya Kabo Verde na Guinea-Bissau, hivi kwamba wataalamu wengi wanadhani ilizaliwa katika pwani za Afrika Magharibi[2][3].

  1. Papiamentu language at Ethnologue
  2. Romero, Simon. "Willemstad Journal: A Language Thrives in Its Caribbean Home", The New York Times, 2010-07-05. 
  3. Lang, George (2000). Entwisted Tongues: Comparative Creole Literatures (kwa Kiingereza). Rodopi. ISBN 9042007370.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search