Kitagalog

Kitagalog ni lugha ya Kiaustronesia nchini Ufilipino inayozungumzwa na Watagalog. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kitagalog iko katika kundi la Kifilipino.

Mwaka wa 2010 idadi ya wasemaji wa Kitagalog nchini Ufilipino imehesabiwa kuwa watu milioni 22.5. Pia, kuna wasemaji 1,600,000 nchini Marekani (2013), walau 500,000 Saudia, 384,000 nchini Kanada (2011) n.k.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search