Korsou

Ramani ya Curaçao
Handelskade in Willemstad, Curaçao

Korsou au Curaçao ni nchi ya visiwani karibu na pwani ya Venezuela (Amerika Kusini).

Tangu mwaka 1634 ilikuwa koloni la Uholanzi; sasa ni "nchi ya kujitawala" ndani ya muundo wa "Ufalme wa Nchi za Chini" pamoja na Uholanzi yenyewe na nchi nyingine mbili za Karibi zilizokuwa makoloni ya Uholanzi (Aruba na Sint Maarten).

Katika eneo la kilometa mraba 444 wanaishi watu 160,012 (2018).

Wengi wao wanatokana hasa na watumwa kutoka Afrika, lakini wana mchanganyiko mkubwa wa damu.

Lugha yao ya kawaida ni Kipapiamentu (81.2%), ambacho ni lugha rasmi pamoja na Kiholanzi na Kiingereza.

Upande wa dini, 72.8% ni Wakatoliki, 16.7% ni Waprotestanti.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search