Mafuta ya petroli

Chupa cha mafuta ya petroli; chupa chenyewe ni cha plastiki inayotengenezwa na mafuta hii
Pampu ya mafuta ya petroli

Mafuta ya petroli (pia petroliamu kutoka Kilatini petra = mwamba na oleum = mafuta au mafuta ghafi) ni kiowevu kizito chenye rangi nyeusi hadi ya kijani. Inatokea kiasili katika ardhi na inawaka rahisi.

Ni chanzo cha petroli, fueli mbalimbali, dawa nyingi na plastiki: hivyo ni kati ya vyanzo muhimu kabisa vya nishati vinavyotumiwa na binadamu kama fueli ya usafiri na ya kutengeneza umeme.

Kikemia mafuta ya petroli ni mchanganyiko wa dutu, hasa hidrokaboni mbalimbali. Inatumiwa kwa njia ya ukenekaji (distillation) ikipashwa moto na sehemu zake kutenganishwa zikifikia kiwango cha kuchemka kwa nyakati mbalimbali.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search