Mashahidi wa Yehova

Makao makuu ya kimataifa huko Brooklyn, New York, Marekani.


Mashahidi wa Yehova (kwa Kiingereza Jehovah's Witnesses) ni wafuasi wa dini jamii ya Ukristo ambayo ilianzia Marekani na kuenea ulimwenguni kote.

Tofauti na Wakristo karibu wote, hao hawamuamini Yesu kuwa Mungu sawa na Baba, wala Roho Mtakatifu kuwa nafsi, na kwa jumla hawakubali imani katika Utatu wa nafsi katika Mungu pekee. Kwa sababu hiyo madhehebu mengi hayawatambui kama Wakristo wala hayakubali ubatizo wao.

Mwanzilishi alikuwa Charles Taze Russell pamoja na kikundi cha wanafunzi wa Biblia (miaka ya 1870). Jina la sasa lilianza kutumika mwaka 1931.

Kwa sasa wako milioni 8.7 katika jumuia 120,387.[1]

Kwa sababu hizo katika nchi mbalimbali dini hiyo iliwahi kukatazwa, kama nchini Tanzania wakati wa urais wa Julius Nyerere au bado ni marufuku.

  1. 2020 Jumla Kuu

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search