Matamshi

Sehemu zinazohusika na matamshi.

Matamshi (kutoka kitenzi "kutamka") ni namna au jinsi watu wanasema hali halisi maneno ya lugha fulani, ambayo inaweza kuwa tofauti na namna ya kuandika neno. Utafiti wa utamshi au utamkaji ni kazi ya somo la fonetiki, tawi mojawapo la isimu.

Matamshi yanaweza kutofautiana kati ya eneo na eneo, na hata kati ya mtu na mtu kulingana na alikoishi utotoni, makazi yake ya sasa, shida katika kutoa sauti[1], kabila, dini, tabaka la kijamii, elimu[2] n.k.

Pengine tofauti hizo husababisha lahaja.

  1. Beech, John R.; Harding, Leonora; Hilton-Jones, Diana (1993). "Assessment of Articulation and Phonology". Katika Grunwell, Pam (mhr.). Assessment in Speech and Language Therapy. CUP Archive. uk. 55. ISBN 0-415-07882-2.
  2. Paulston, Christina Bratt; Tucker, G. Richard (Februari 14, 2003). "Some Sociolinguistic Principles". Katika Labov, William (mhr.). Sociolinguistics: The Essential Readings. Wiley-Blackwell. ku. 234–250. ISBN 0-631-22717-2.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search