Milima kunjamano

Bamba la gandunia A linasukumwa chini ya bamba la gandunia B; shinikizo kwenye kona ya B inasababisha kupanda kwa milima kunjamano. Kona ya A inatelemka katika magma C ya koti ya dunia na kuyeyuka.
Mgongano wa mabamba mawili hujenga milima kunjamano
Safu sambamba za Rocky Mountains (Marekani)

Milima kunjamano (kwa Kiingereza fold mountains) ni aina ya milima ambayo hutokea wakati mabamba ya gandunia yanagongana. Shinikizo linasababisha kukunjwa kwa ganda la dunia na hili linafanya sehemu ya uso wa ardhi kuinuliwa juu.

Tokeo lake ni safu ya milima au pia mfululizo wa masafu yaliyo sambamba.

Milima kunjamano ni umbo la kawaida kati ya milima mirefu duniani. Mifano ni milima ya Atlas katika Afrika ya Kaskazini, Alpi katika Ulaya na Himalaya katika Asia. Kilimanjaro ni mlima mrefu kwa upande wa Afrika lakini si mlima kunjamano kwa sababu ni volkeno ya pekee.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search