Misia


Mahali pa Misia.

Misia (kwa Kigiriki: Μυσία, Mysía; kwa Kituruki: Misya) ilikuwa eneo la Asia Ndogo ya zamani, kaskazini magharibi mwa rasi ya Anatolia (leo nchini Uturuki).

Ilipakana na Bahari ya Marmara, Bitinia, Frigia, Lydia, Eolia, Troa na Proponto, ingawa mipaka yake ilibadilikabadilika.

Kati ya miji yake, muhimu zaidi ulikuwa Pergamo.

Inatajwa na Matendo ya Mitume (16:7-8) katika kusimulia safari ya pili ya kimisionari ya Mtume Paulo.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search