Mjao

Mjao (kwa Kiingereza volume) unaeleza ukubwa wa gimba la hisabati (mchemraba, tufe, mcheduara) kwa kupima nafasi ya yaliyomo yake.

Hupimwa katika vizio vya ujazo kama mita ujazo (m³) au sentimita ujazo (cm³).

Kila gimba lenye urefu, upana na kimo huwa na mjao.

Alama yake ni V.

Hali halisi ni kwamba nje ya hisabati kuna njia mbili za kuangalia mjao wa gimba:

  • ujazo wa nje kwa jumla (kwa mfano kama kitu kinazamwa katika kiowevu kinasukuma kiasi gani cha kiowevu hiki?)
  • ujazo wa ndani (kwa mfano yaliyomo ya boksi au tangi)

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search