Mona Lisa

Mchoro wa Mona Lisa, uliofanywa na Leonardo da Vinci.

Mona Lisa (pia huitwa La Gioconda ambayo kwa Kiitalia ina maana ya mwanamke mchangamfu) ni mchoro maarufu wa mwanzoni mwa karne ya 16, kazi ya mwanasayansi na mchoraji Leonardo da Vinci.

Inaaminika kuwa ni mmoja kati ya michoro mashuhuri zaidi duniani kote. Kwa sasa mchoro huu unapatikana katika jumba la maonyesho (makumbusho) la jijini Paris (Ufaransa) maarufu kama Louvre.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search