Montserrat

Plymouth, mji mkuu wa zamani na bandari kuu ya Montserrat, tarehe 12 Julai 1997, wakati wa mlipuko mpya wa volkeno.

Montserrat ni eneo la ng'ambo la Ufalme wa Muungano lililopo katika Karibi.

Ni kisiwa chenye urefu wa kilometa 16 na upana wa kilometa 11, kikiwa na kilometa 40 hivi za pwani.

Kwa jumla ni kilometa mraba 102 wanakoendelea kuishi watu 4,900 baada ya wengi zaidi kuhama kutokana na milipuko ya volkeno iliyotokea kuanzia mwaka 1995 baada ya karne kadhaa za utulivu.

Wananchi wengi wanatokana na watumwa kutoka Afrika na kutoka Eire waliozaliana zamani za ukoloni wa Waingereza.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search