Motokaa

Ford Mondeo ni motokaa ndogo ya kubeba abiria wachache, kwa mfano familia ndogo.
Magari kama Toyota Landcruiser hujengwa juu ya fremu ya lori dogo kwa kusudi la kubeba watu kwenye njia mbaya.

Motokaa (kutoka Kiingereza "motor car"[1], mara nyingi huitwa tu gari kutoka neno la Kihindi) ni chombo cha usafiri ambacho kwa kawaida kinakwenda kwenye nchi kavu kikitumia nguvu ya injini au mota yake. Hata hivyo ziko zinazoweza kusafiri pia majini, na kwa sasa kampuni kadhaa duniani zinafanya utafiti wa kutengeneza motokaa ambazo zitakuwa zikiruka angani.

Kuna aina nyingi za motokaa: magari madogo hubeba abiria tu na gari dogo la kawaida hubeba dereva pamoja na abiria hadi wanne. Magari makubwa kidogo hubeba hadi watu 8.

Mengine ya kubeba abiria ni mabasi ambayo ni pia aina ya motokaa lakini mara nyingi hutajwa kama kundi la pekee, sawa na malori ambayo ni motokaa kubwa za kubeba mizigo. Kuna kila aina ya mchanganyiko kati ya aina hizi.

Fremu ya motokaa pamoja na magurudumu, bila injini wala bodi.
  1. Maneno hayo yana asili katika lugha ya Kilatini; "car" kutoka Kilat. carrus = gari na "motor" kutoka Kilat. movere = sogeza, hamisha yaani "mhamishaji, msukumaji"

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search