Mutilene (kwa Kigiriki: Μυτιλήνη, Mytilíni) ni mji wa Ugiriki, makao makuu ya kisiwa cha Lesbo katika Bahari ya Aegean chenye eneo la Km² 1,633.
Una wakazi 29,656 (2011) wanaotegemea zaidi uvuvi na utalii.
Mwaka 58 Mtume Paulo, katika safari yake ya tatu ya kimisionari, aliabiri kutoka huko hadi Samos akielekea Yerusalemu[1].
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search