Muziki wa Kikristo

Kwaya ya Ethiopia mbele ya ukuta wa picha.


Muziki wa Kikristo ni muziki uliotungwa ili kutokeza imani ya Ukristo katika sanaa hiyo, kwa mfano katika kumsifu Mungu, kumshangilia Yesu Kristo, na kuomba msamaha wa dhambi.

Hivyo, tofauti na miziki mingine, lengo kuu si kuburudika na uzuri tu.

Namna zake ni tofautitofauti kadiri ya nyakati, madhehebu, utamaduni n.k. Mojawapo, kati ya zile za zamani zaidi, inaitwa muziki wa Kigregori, kwa sababu iliagizwa na Papa Gregori I itumike kanisani.

Matumizi makubwa zaidi ni yale ya ibada, ambapo waamini waliokusanyika wanaimba pamoja, mara nyingi wakiongozwa na kwaya na wakisindikizwa na ala za muziki.

Matumizi mengine ni wakati wa kutoa mahubiri na mafundisho hata barabarani.

Pengine yanafanyika makongamano maalumu kwa wapenzi wa muziki huo, na vilevile siku hizi unarekodiwa kwa vifaa vya teknolojia hata kwa matumizi ya mtu binafsi.

Kwaya ikiimba kanisani huko Ulaya.
Mwimbaji Darlene Zschech.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search