Nembo ya Kenya

Nembo ya Kenya

Nembo ya Kenya huonyesha simba wawili wanaoshika mishale na ngao ya Maasai. Ngao huoneyesha rangi za taifa zilizogawanyika katika sehemu nne.

  • Nyeusi humaanisha watu wazaliwa Kenya
  • Kijani humaanisha kilimo na maliasili
  • Nyekundu humaanisha mapambano kupata uhuru
  • Nyeupe humaanisha umoja na usalama

Sehemu nyekundu huonyesha jogoo anayeshika shoka; hii humaanisha maisha bora. Ngao na simba wamesimama juu ya Mlima Kenya. Chini ya ngao kimeandikwa Harambee.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search