Orange Democratic Movement

Orange Democratic Movement
IdeologyDemocracy, Reform, Constitutionalism
Orange Democratic Movement
Jina kamiliORANGE DEMOCRATIC MOVEMENT
Jina la utanichama cha chungwa, Chungwa, orange
ImeanzishwaMachi 10, 2007 (2007-03-10)
MmilikiRaila Odinga
MwenyekitiJohn Mbadi

Orange Democratic Movement (ODM) (jina kamili: Orange Democratic Movement Party of Kenya) ni chama cha kisiasa nchini Kenya. Kilianzishwa mwaka 2006 katika maandalizi ya uchaguzi wa bunge la Kenya wa mwaka 2007, lakini asili yake ni harakati za kura juu ya katiba mpya nchini Kenya ambayo ilianzishwa mwaka 2005 kwa ajili ya kura ya maoni ya katiba ya Kenya.

ODM ilianzishwa na chama cha Uhuru Kenyatta, KANU na chama cha Raila Odinga, LDP, lakini chama cha KANU kiliweza kujiondoa, na waliobaki waligawanyika katika makundi haya mawili yanayoongozwa na Raila Odinga (ODM; ndio wengi zaidi) na Kalonzo Musyoka (ODM-Kenya). Sababu ya farakano ilikuwa suala la nani atakuwa mgombea wa urais upande wa ODM.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search