Pafo


Nguzo ya Mtume Paulo huko Pafo.

Pafo (kwa Kigiriki cha zamani: Πάφος [ˈpafos]; kwa Kituruki: Baf) ulikuwa mji mkuu wa kisiwa cha Cyprus wakati wa Dola la Roma. Kwa sasa ni makao makuu ya wilaya ya Pafo.

Pafo ilifikiwa na wamisionari Mtume Paulo na Barnaba mwaka 45 hivi (Mdo 13:4-12). Katika nafasi hiyo, liwali Sergius Paulus aliongokea Ukristo.

Mji huo umeorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search