Pijini

Pijini ni lugha ambayo hutokea pale ambapo wazungumzaji wa lugha mbili tofauti hukutana; hapo, ili kukidhi haja yao ya kuwasiliana, inawalazimu kuibua au kutumia lugha moja ambayo itawawezesha kuelewana katika nyanja za mawasiliano.

Kwa maneno mengine, pijini ni lugha ambayo huzuka pale ambapo makundi mawili ya watu wenye lugha mbalimbali yanapokutana na haja ya mazungumzo hutokea. Mara nyingi ni lugha za biashara hasa.

Pijini kadhaa zinazoonekana leo zilianza wakati wa ukoloni ambako watu waliotawaliwa na mataifa ya Ulaya kwa hiari yao au kwa kulazimishwa walianza kutumia lugha ya Kizungu katika maisha ya kila siku.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search