Plastiki

Vifaa vya nyumbani vilivyotengenezwa kwa plastiki

Plastiki (kutoka Kigiriki πλαστική plastiki yaani "iliyopewa umbo fulani" ) ni aina ya maunzi mango yanayoundwa kwa njia ya kikemia na kukubali umbo lolote yakiwa teke.

Plastiki ni maunzi sintetiki ambayo haitokei katika mazingira kiasili. Inatengenezwa kwa kuunganisha molekuli nyingi kuwa nyororo ndefu ya polima.

Kuna aina nyingi za plastiki. Kwa kuchagua kemikali na kuongeza madawa mbalimbali kuna chaguo kubwa ya tabia kama ugumu, kubadilika umbo, unyumbufu, uvumilivu kwa joto au baridi au muda wa kudumu.

Wakati wa kutengenezwa plastiki inakubali kila umbo hivyo hutolewa kama filamu, punje, vipande bapa au umbo lolote linalotakiwa. Mifuko na maunzi ya kufugia bidhaa huwa ni plastiki. Plastiki haipokei maji au unyevu hivyo kitu kinachofungwa kabisa ndani ya karatasi ya plastiki inabaki kavu.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search