Pua

Pua ya binadamu.
Kono la tembo ni pua ndefu.

Pua ni kiungo cha mwili wa watu na wanyama vertebrata chenye tundu kilicho juu ya mdomo. Kazi yake ni kunusa harufu ya vitu.

Inasaidia pia kazi ya kupumua; tena kwa wanyama kadhaa kama farasi ni mlango mkuu wa mfumo wa upumuaji.

Kwa watu na pia wanyama wengi puani mna nywele zenye kazi ya kuchuja vumbi.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search