Santo Domingo

Santo Domingo

Santo Domingo ya kihistoria (Kanisa Kuu)
Habari za kimsingi
Utawala Wilaya ya Kitaifa (Distrito Nacional)
Anwani ya kijiografia Latitudo: 18°30′N - Longitudo: 69°59′W
Kimo 14 m juu ya UB
Eneo - 80 km²
Wakazi - mji: 913,540 (2001)
- rundiko la mji: 2,500,000
Msongamano wa watu watu 1,141 kwa km²
Simu +1809 (nchi yote)
Mahali

Santo Domingo ni mji mkuu wa Jamhuri ya Dominikana. Ni kati ya miji ya kale kabisa ya Karibi: ilikuwa mji wa kwanza ulioanzishwa na Wahispania katika Amerika. Kuna majengo ya kwanza ya historia ya kikoloni katika Amerika yote yaani kanisa la kwanza, chuo kikuu cha kwanza na hospitali ya kwanza.

Idadi ya wakazi ni mnamo milioni mbili.

Wakati wa udikteta wa Rafael Trujillo mji uliitwa "Ciudad Trijillo" (mji wa Trujillo) kati ya miaka 1936 hadi 1961.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search