Sifuri

Tarakimu sifuri.

Sifuri (au sufuri kutoka Kiarabu sifr iliyotafsiri neno la Kisanskrit sunya lenye maana ya mahali patupu) ni namba ya pekee ambayo haina thamani peke yake, mpaka iandikwe baada ya namba nyingine yoyote: hapo inazidisha thamani yake mara kumi. Kwa kawaida inaandikwa 0 lakini ٠ kwa namba za Kiarabu.

Kwa Kiswahili namba hiyo inaitwa pia ziro kutokana na neno hilohilo la Kiarabu lakini kwa kupitia Kiitalia, Kifaransa na hatimaye Kiingereza (inapoandikwa zero).

Sifuri kama namba ilianza kutumika India kabla ya karne ya 9 BK, pengine hata karne ya 3.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search