Skauti (kutoka neno la Kiingereza "scout") ni mtoto, kijana au msichana anayewajibika katika chama cha kimataifa, akivaa sare kama ya askari mdogo na kukaa katika safu.
Pia ni chama kisicho cha kiserikali kinachomjenga kijana katika maadili mema na ya kujituma na kusaidia watu katika maisha yao.
Chama hicho hakibagui vijana kwa msingi wa jinsia, umri, dini, rangi wala kabila.
Skauti huhitajika kuwepo kwa kila shule za sekondari duniani.
Mwanzilishi wa uskauti duniani (1907) alikuwa Robert Baden-Powell (1857–1941) kutoka Uingereza. Lengo lake lilikuwa kusaidia vijana kukua vizuri pande zote (mwili, nafsi na roho) ili hatimaye wawe raia wema katika jamii. Leo hii wako skauti milioni waliounganisha katika makundi na vyama vingi; idadi kubwa aidi nni wanachama katika Shirika la Harakati za Skauti Duniani linalounganisha skauti milioni 57[1] kote duniani.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search