| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: Nad Tatrou sa blýska ("Radi juu ya milima ya Tatra") | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Bratislava | ||||
Mji mkubwa nchini | Bratislava | ||||
Lugha rasmi | Kislovakia | ||||
Serikali | Democrasia Peter Pellegrini Robert Fico | ||||
Uhuru kutoka Chekoslovakia |
tarehe 1 Januari 1993 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
49,037 km² (ya 130) -- | ||||
Idadi ya watu - 2023 kadirio - 2022 sensa - Msongamano wa watu |
5,424,687 (ya 119) 5,460,185 111/km² (ya 104) | ||||
Fedha | EURO (€ )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .sk2 | ||||
Kodi ya simu | +4213
- |
Slovakia (Kwa Kislovakia Slovenská republika), rasmi kama Jamhuri ya Slovakia, ni nchi isiyo na pwani katika Ulaya ya Kati, inayopakana na Poland kaskazini, Ukraini mashariki, Hungaria kusini, Austria kusini-magharibi, na Jamhuri ya Czech magharibi. Ina idadi ya watu takriban milioni 5.4, ikiwa ya 117 duniani. Jiji lake kubwa zaidi na mji mkuu ni Bratislava. Slovakia imegawanyika katika mikoa 8 (kraj). Inajulikana kwa milima yake ya Tatras, majumba ya kihistoria, na mchanganyiko wake wa utamaduni wa Kislavic na Kati ya Ulaya.
Slovakia imekuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004.
Miji muhimu baada ya Bratislava ni Košice, Banská Bystrica, Žilina, Trenčín, Nitra, Prešov na Trnava.
Wakazi walio wengi wanasema Kislovakia, ambacho ni kati ya lugha za Kislavoni, lakini kieneo kuna pia wasemaji wa Kihungaria, Kibelarus na Kiukraine.
Upande wa dini, 65.8% ni Wakatoliki, 8.9% Waprotestanti. 13.4% wanajitambulisha kama Wakanamungu.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search