Spika

Spika (kutoka Kiingereza "speaker" msemaji) ni cheo cha mwenyekiti wa bunge katika nchi zinazofuata urithi wa kisiasa wa Uingereza. Nchi nyingi zilizokuwa koloni za Uingereza kama vile Marekani, Uhindi, Tanzania, Kenya, Nigeria, Australia au New Zealand huwa na cheo hiki hasa zikitumia lugha ya Kiingereza kama lugha rasmi. Neno la Kiingereza limepokelewa pia katika lugha ya Kiswahili.

Katika nchi zisizo na urithi wa Kiingereza vyeo kama mwenyekiti au rais wa bunge hutumiwa.

Kazi yake ni kuratibu shughuli na majadiliano ya bunge. Huamua juu ya maswali ya utaratibu bungeni, ufuatano wa wabunge katika majadiliano , kutangaza matokeo ya kura bungeni na kadhalika. Ndiye mwakilishi wa bunge kwa ujumla.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search