Tano

Mabadiliko katika kuandika tano.

Tano ni namba ambayo inafuata nne na kutangulia sita. Kwa kawaida inaandikwa 5 lakini V kwa namba za Kiroma na ٥ kwa zile za Kiarabu.

5 ni namba tasa.

Neno hilo lina asili ya Kibantu. Kiswahili kina neno lingine kwa maana hiyohiyo, nalo lina asili ya Kiarabu: hamsa. Siku hizi halitumiki sana, lakini kutoka kwake limepatikana hamsini (hamsa mara kumi) ambalo ni la kawaida.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search