Tufe

Picha ya tufe
Rediasi au nusukipenyo (= r) cha tufe

Tufe ni umbo la gimba linalofanana na mpira au chungwa. Lakini wala mpira wala chungwa ni tufe kamili.

Katika elimu ya hisabati, hasa jiometri tufe ni jumla la nukta zote zilizopo na umbali uleule (=rediasi, nusukipenyo) kutoka nukta nukta moja (kitovu cha tufe).

Tufe ni mzunguko wa duara katika wanda (dimension) la tatu.

  • Kitovu cha tufe ni nukta iliyopo katikati yake yenye umbali sawa na kila nukta kwenye uso wake.
  • Nusukipenyo cha tufe ni umbali kati ya kitovu chake hadi nukta yoyote kwenye uso wake
  • Uso wa tufe ni eneo linalojumlisha nukta zote zenye umbali wa nusukipenyo kutoka kitovu

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search