Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2005

Uchaguzi wa mwaka 2005 ulimweka Jakaya Kikwete madarakani.
Tanzania

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Tanzania



Zanzibar

Nchi zingine · Atlasi

Nchi ya Tanzania ilifanya uchaguzi wa urais na ubunge mnamo 4 Desemba 2005. Mapema ulikuwa ulipangiwa kufanyika mnamo 30 Oktoba lakini ukahairishwa kutokana na kifo cha mgombea kiti cha Makamu wa Rais. Uchaguzi huu ulikuwa wa tatu tangu nchi hiyo kurudia mfumo wa vyama vingi mnamo 1992. Pia ulikuwa wa pekee kwa kuwa aliyekuwa rais, Benjamin Mkapa, ambaye alikuwa amehudumu kwa kipindi cha miaka kumi alistaafu kulingana na Katiba. Uchaguzi wa Urais wa Zanzibar na wawakilishi katika jumba la wawakilishi ulifanyika mnamo 30 Oktoba, jinsi ilivyokuwa imepangwa.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search