Ufalme wa Kikatiba

Ufalme wa kikatiba ambako mfalme ni kiongozi wa heshima tu yanaonyeshwa kwa rangi nyekundu. Rangi ya dhambarau inaonyesha nchi ambako mfalme ana athira kubwa chini ya katiba. Nchi ya Uthai ina mfalme na katiba lakini katiba imepumzishwa kwa sasa na serikaliy a kijeshi (2006/2007).

Ufalme wa Kikatiba ni muundo wa serikali ambako kaisari, sultani, mfalme, malkia au mtemi ni mkuu wa nchi chini ya katiba yake. Hii inamaanisha ya kwamba madaraka ya mfalme yana mipaka yao katika masharti za katiba na sheria za nchi. Pale ambako hakuna katiba ya kimaandishi inayoratibu mambo mengi kuna kawaida inayoweka mipaka kwa madaraka ya mfalme jinsi ilivyo Uingereza.

Madaraka ya mfalme katika muundo huu yanatofautiana sana.

Zamani wafalme walikuwa mara nyingi viongozi wenye madaraka yote wasiobanwa na bunge au sheria. Aina hii ya ufalme umebaki mahali pachache tu kwa mfano Saudia.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search