Ufunuo

Ufunuo ndio tukio au mchakato ambao mawasiliano kati ya Mungu na binadamu yanafanyika. Ufunuo ni pia yaliyomo katika ujumbe unaotokana na Mungu.

Ni kwamba katika dini mbalimbali kuna imani ya kwamba Mungu anaweza kujifunua kwa binadamu na kuwafunulia matakwa yake kwao.

Pengine ufunuo huo unakuja kuandikwa katika kitabu kitakatifu, kama vile Biblia kwa Wayahudi na Wakristo, na Torati, Zaburi, Injili na Kurani kwa Waislamu.

Ufunuo una umuhimu mdogo katika dini nyingine, isipokuwa katika Ubuddha.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search